SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA- NAFASI ZA KAZI 43 SHIRIKA LA MZINGA

JAMHURI YA MUUNGANO
WA
TANZANIA OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA
AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Ref.No.EA.7/96/01/J/31
13 Septemba, 2017
TANGAZO
LA
NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Shirika la
Mzinga anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 43 kama zilivyoainishwa hapa chini.
1.0 SHIRIKA LA MZINGA
Shirika la Mzinga ni Taasisi ya Serikali
chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa.
Waombaji wa nafasi za kazi katika Shirika la Mzinga watambue kituo chao cha kazi ni
Makao Makuu ya Shirika:-
1.1 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (FITTER AND TURNER) -NAFASI 12
1.1.1 MAJUKUMU YA FUNDI MCHUNDO DARAJA II (FITTER AND TURNER)
i. Kuchonga vipuri mbalimbali;
ii. Kusoma na kutafri michoro mbalimbali inayotumika katika karakana;
iii. Kuhakikisha hali ya usafi na usalama mahala pa kazi;
iv. Kuendesha mashine mbalimbali za uchongaji katika karakana kama vile Lathe, Milling, Grilling, Drilling nk;
v. Kufanya kazi za fitting;
vi. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vii. Kufanya kazi
nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi
wake.
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti
cha Ufundi Stadi (Trade Test Grade III/CBET I) yenye mwelekeo wa ‘Fitter and Turner’ kutoka
VETA
au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2.
1.2 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (FITTER
MECHANICS) -NAFASI 8
1.2.1 MAJUKUMU YA FUNDI MCHUNDO DARAJA II (FITTER MECHANICS)
i. Kufanya uchunguzi ili kutambua chanzo cha tatizo na kutoa taarifa kwa ajili ya
maamuzi;
ii. Kufanya matengenezo ya mitambo mbalimbali ya Shirika;
iii. Kuhakikisha mitambo ipo katika hali nzuriwakati wote;
iv. Kuendesha mitambo;
v. Kukagua na kutambua vipuri na vijenzi vilivyoharibika (worn parts) kwa kufuata ratiba ya matengenezo;
vi. Kusoma na kutafri michoro mbalimbali ya mifumoya mashine; vii.
Kubadilisha vipuri vilivyoharibika katika mashine na mitambo; viii.
Kufanya ‘marking –off’ kulingana na michoro;
ix. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
x. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa ‘Fitter Mechanics’
kutoka VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
1.2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.3 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (MCHOMELEAJI) -
NAFASI 4
1.3.1 MAJUKUMU YA FUNDI MCHUNDO DARAJA II (MCHOMELEAJI)
i. Kukarabati mashine;
ii. Kuunda mashine;
iii. Kuunga na kukata vyuma;
iv. Kuchora michoro
(Free hand Sketch) na kutafsiri michoro mbalimbali;
v. Kufanya uungaji kwa kutambua aina mbalimbali za miungo;
vi. Kushirikiana
na
wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vii. Kufanya kazi
nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi
wake.
1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa kulehemu ‘welding’ kutoka VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
1.3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.4 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (USUBIAJI NA UUNGAJI VYUMA-MOULDING) - NAFASI 2
1.4.1
MAJUKUMU YA
FUNDI
MCHUNDO DARAJA II (USUBIAJI
NA UUNGAJI VYUMA-MOULDING)
i. Kuandaa mchanga utumikao katika uandaaji wa ‘moulds’
na
‘core’ mbalimbali;
ii. Kutengeneza ‘moulds’ za aina mbalimbali kwa ajili ya usubiaji;
iii. Kusubu brasi na vyuma;
iv. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
v. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa Usubiaji na Uungaji Vyuma ‘moulding’ kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.4 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (UUNDAJI WA PATENI) -NAFASI 1
1.4.1 MAJUKUMU YA FUNDI MCHUNDO DARAJA II (UUNDAJI WA PATENI)
i. Kusoma na kutafsiri michoro;
ii. Kutambua tabia mbalimbali za mbao zinazotumika kutengenezea pateni;
iii. Kutengeneza pateni na ‘core
boxes;
iv. Kukarabati pateni na ‘core boxes’;
v. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vi. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.4.2 1.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa Uundaji waPateni ‘Pattern Maker’ kutoka VETA au Chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.5 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (UMEME) -
NAFASI 1
1.5.1
MAJUKUMU YA FUNDI
MCHUNDO DARAJA II (UMEME) i. Kusoma na kutafsiri mifumo (wiring)
mbalimbali ya umeme;
ii. Kufanya ‘wiring’ za taa na mitambo;
iii. Kufanya matengenezo ya mifumo ya umeme;
iv. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
v. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa Ufundi Umeme
kutoka VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
1.5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.6 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (USEREMALA-CARPENTRY AND JOINERY) - NAFASI 2
1.6.1
MAJUKUMU YA FUNDI MCHUNDO DARAJA II (USEREMALA-CARPENTRY
AND
JOINERY)
i. Kuchambua na kushauri juu ya matumizi
ya
aina mbalimbali ya mbao;
ii. Kutengeneza samani na mazao yatokanayo na mbao;
iii. Kufanya ukarabati mbalimbali wa samani na kazi zinahusu mbao;
iv. Kukagua na kutoa taarifa ya maeneo yanayohitaji matengenezo;
v. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vi. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa Useremala –‘Carpentry
and
Joinery’ kutoka VETA au Chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.7 FUNDI MCHUNDO DARAJA II
(FUNDI
MAGARI-MOTOR VEHICLE
MECHANICS) -NAFASI 6
1.7.1
MAJUKUMU YA
FUNDI
MCHUNDO
DARAJA II (FUNDI
MAGARI-MOTOR
VEHICLE MECHANICS)
i. Kufanya matengenezo kinga (Preventive maintenance) ya ‘Clutch’, ‘Gear boxes’
mifumo ya breki nk;
ii. Kuchunguza
na kutambua
matatizo ya magari na mitambo na kufanya
matengenezo;
iii. Kufanya majaribio ya ubora
wa
magari na mitambo baada ya matengenezo;
iv.
Kuhakikisha
utunzaji wa
zana
zinazotumika
katika karakana za
magari
na mitambo;
v. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vi. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi
wake.
1.7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa Ufundi Magari- ‘Motor Vehicle Mechanics’
kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Mashirika ya Umma PGSS 2
1.9 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (FUNDI BOMBA) -NAFASI 1
1.9.1 MAJUKUMU
YA
FUNDI MCHUNDO DARAJA II (FUNDI
BOMBA)
i. Kuchora na kutafsiri
michoro ya mifumo ya mabomba;
ii. Kufanya makadirio ya gharama za matengenezo ya bomba;
iii. Kuhakikisha usalama na usafi
wa
mabomba kadri ya viwango nvya ubora;
iv. Kufanya ukarabati
na
matengenezo ya mifumo ya mabomba;
v. Kufanya ukaguzi na kushauri juu ya mifumo ya mabomba ya maji na maji taka;
vi. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vii. Kufanya kazi
nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi
wake.
1.9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha
Ufundi Stadi
(Trade Test Grade III/CBET
I) yenye mwelekeo wa Ufundi Bomba kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.10 FUNDI MCHUNDO
DARAJA II (UASHI) - NAFASI 2
1.10.1 MAJUKUMU YA FUNDI
MCHUNDO DARAJA II (UASHI)
i. Kutunza vifaa na zana za ujenzi
katika hali ya usafi na usalama;
ii. Kufanya ujenzi
wa
majengo kwa kufuata
michoro;
iii. Kukarabati majengo;
iv. Kufanya makadirio ya gharama za ujenzi;
v. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vi. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti
cha Ufundi
Stadi (Trade Test Grade III/CBET I)
yenye
mwelekeo wa Uashi kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
ya
Mashirika ya Umma PGSS 2
1.11 MTEKNOLOJIA DARAJA LA II – MAABARA -NAFASI 1
1.11.1 MAJUKUMU YA MTEKNOLOJIA DARAJA LA II
i. Kupima sampuli zinazoletwa maabara;
ii. Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi;
iii. Kufanya kazi za ukaguzi wa maabara, vitendanishi, vifaa, kemikali na hifadhi ya
kemikali;
iv. Kuweka kumbukumbu za maabara ambazo zimepatikana wakati
wa uchunguzi;
v. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika;
vi. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Stashahada katika fani
ya Uteknolojia/Ufundi
Sanifu
Maabara katika
Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara za watumishi wa kada za tiba wa taasisi za Serikali
PMGSS 2
1.12 MHUDUMU WA
AFYA DARAJA LA II – NAFASI 1
1.12.1 MAJUKUMU YAMHUDUMU WA
AFYA DARAJA LA II:
i. Kufanya usafi
wa
vifaa vya kazi, usafi
wa
wodi na mazingira;
ii. Kusaidia wagonjwa wenye ulemavu na wasiojiweza katika kwenda haja (kubwa na ndogo) na kuoga;
iii. Kumsaidia kumlisha mgonjwa asiyejiweza;
iv. Kuchukua nguo za mgonjwa kuzipeleka kwenda kufuliwa;
v. Kuchukua sampuli za mgonjwa kwa ajili ya vipimo vya maabara na kufuatilia majibu;
vi. Kutayarisha vifaa kwa ajili ya kusafisha na kufunga majeraha;
vii. Kufuatilia mahitaji ya dawa kwa wagonjwa kutoka hifadhi
ya
dawa;
viii. Kufanya kazi
nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi
wake.
1.12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kidato cha nne na mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya uuguzi katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara za watumishi wa kada za tiba wa taasisi za Serikali
PMOSS 1
1.13 KATIBU MUHTASI DARAJA LA III
NAFASI 1
1.13.2 MAJUKUMU YA KATIBU MUHTASI DARAJA LA III
i. Kuchapa barua/taarifa na nyaraka za kawaida;
ii. Kusaidia kupokea wageni, kuwasaili
shida zao na
kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
iii. Kusaidia kutunza
taarifa/kumbukumbu
za matukio,
mihadi, wageni
tarehe za
vikao safari za mkuu wake na ratiba za kazi
zingine;
iv.
Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi
kwa wasaidizi wake ofisini;
v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake ofisini;
vi. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.
1.13.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kidato cha nne, mafunzo ya uhazili hatua ya tatu na mafunzo ya kompyuta katika chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
1.13.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi
za mishahara
za
watumishi wa Taasisi za Serikali PGSS 1
1.14 MTEKNOLOJIA DARAJA II – FAMASI
(NAFASI 1)
1.14.1 MAJUKUMU YA MTEKNOLOJIA DARAJA LA II
i. Kuainisha, kuandaa, kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo lake la
kazi;
ii. Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa na watumishi;
iii. Kuchanganya dawa;
iv. Kuhifadhi dawa na vifaa tiba;
v. Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi
ya
dawa;
vi. Kukagua dawa, vifaa tiba kemikali,
vitendanishi na vipodozi katika eneo lake la
kazi;
vii. Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa;
viii. Kuandaa taarifa ya matumizi
ya
dawa na vifaa tiba;
ix. Kufanya uchunguzi
wa
ubora wa
dawa, vifaa
tiba
kemikali,
vitendanishi
na vipodozi
x. Kufanya kaguzi mbalimbali katika sehemu zinazohifadhi dawa;
xi. Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba;
xii. Kufanya kazi
nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi
wake.
1.14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Stashahada katika fani ya Uteknolojia/Ufundi sanifu dawa katika Chuo kinachotambuliwa na
Serikali na
ambao wamesajiliwa (Enrolled) na mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA).
1.14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara za watumishi wa kada za tiba ya Taasisi ya Serikali
PMGSS 1
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI
ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni
Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka
45 ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi
ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja
na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani
wa
kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi
karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV
AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU,
NECTA na NACTE).
viii.
Waombaji waliostaafishwa katika
Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia waliomo katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa ielekezwe kwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi
wa
Umma na inaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi
wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. xii.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni
tarehe 26 Septemba, 2017.
xiii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia
sehemu iliyoandikwa
‘Recruitment Portal’)

No comments: